Jalada la Afisa wa Polisi anayetajwa kwa jina la Fatuma Kigondo limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka- DPP baada ya uchunguzi wa kina kufanyika ikiwa ni pamoja na kupata maelezo ya watu mbalimbali pamoja na afisa Fatuma mwenyewe.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi iliyotolewa leo Jumamosi, Agosti 24, 2024 kupitia msemaji wa jeshi hilo David Misime.
Afisa huyo wa polisi Fatuma Kigondo anatajwa kuwa ndiye ” Afande ” anayeombwa msamaha na binti wa Yombo Dovya jijini Dar es salaam ambaye alibakwa na kuingiliwa kinyume na maumbile na vijana watano huku akirekodiwa ambapo afisa huyo anahusishwa na kuwatuma vijana kumfanyia ukatili binti huyo kwa madai kuwa anatembea na mume wa ” Afande “.
