Kupitia mitandao yake rasmi ya kijamii, Waziri wa Fedha ambaye pia ni mdhamini wa Singida Black Stars ameiomba Yanga kumsamehe Yusuf Kagoma aende Simba anakotaka akacheze kwa maslahi ya kukuza mpira wa Tanzania.
“Nafahamu undani wa suala la Yusuf Kagoma. Ni kweli Kagoma alisaini mkataba Yanga na baadae akasaini Simba. Najua kutokwenda kwake Yanga na badala yake kusaini Simba hata sio masuala ya fedha. Tutatumia muda sana tukitaka kuchimba haya. Kagoma ni mtoto wetu, Yanga ni Club kubwa sana na ina mambo muhimu ya kuyawekea nguvu kuyafanikisha kuliko kuweka nguvu Kagoma aisicheze licha ya ukweli kwamba alistahili achezee Yanga,” ameandika Mwigulu.
Akaendelea: “Nimewaomba viongozi wa Yanga wasamehe yote, waondoe shauri dhidi ya Kagoma, wamwache awe huru akaitumikie Simba kwa maslahi mapana ya mpira wa Tanzania na kwa faida ya mchezaji.”